SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Monday, May 6, 2013

SSPRA YAPATA VIONGOZI WAPYA.

SSPRA imefanya uchaguzi wa viongozi wapya watakaoiendeleza SSPRA mara baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao wa uongozi na kuwapa fulsa wanachama wengine pia kukiendeleza chama. 

Nafasi zilizokuwa zikiwaniwa zilikuwa ni 8 na zote zimepata viongozi wake watakao endeleza pale uongozi uliokuwa chini ya Mwenyekiti Christopher Ngonyani umeishia kwa maendeleo ya chama hiki cha wanafunzi wanaosomea shahada ya mahusiano ya jamii na masoko.Majina ya viongozi wapya ndio haya hapa chini.

MWENYEKITI
Sing'ambi Athanas ndiye Mwenyekiti alipata kura 72 kati ya jumla ya 86, kura 14 zilienda kwa Andrew Geofrey.

MAKAMU MWENYEKITI
Makura Ndege ndiye M/msaidizi alipata kura 59 kati ya jumla ya kura 84 na kura 25 zilienda kwa Chenga Norbert

KATIBU MKUU
Mbwaga Aman E. Ndiye katibu mkuu wa SSPRA alipata kura 66 kati ya kura 88 na 22 zilienda kwa Haule Adam 

KATIBU MSAIDIZI
FURA EPHRAIM LODRICH ndiye katibu msaidizi alipata kura 44 kati ya kura 85, kura 41 zilienda kwa Joseph Michael.

AFISA UHUSIANO (PRO)
Athanas Masota M ndiye afisa uhusiano wa SSPRA alipata kura 75 kati ya kura 85 na kuweza kumshinda Emily Alex aliyepata kura 10 

AFISA UHUSIANO MSAIDIZI
Jesse Edwin ndiye afisa uhusiano msaidizi aliyeshinda kwa kura 69 kati ya kura 88, kura 19 zikaenda kwa Kalumbilo John.

MHASIBU MSAIDIZI
BAHATI WILSON ndiye mhasibu msaidizi ambaye alipigiwa kura ya ndio au hapana kwa kuwa alikuwa peke yake katika nafasi hiyo na kuweza kupigiwa kura 82 za NDIO na kura 2 za HAPANA.   

MHASIBU MKUU 
Kyando Zawadi S. ndiye Mhasibu mkuu aliyemshinda Munuo Hosiana.
viongozi wapya wa SSPRA katika picha ya pamoja

Mwenyekiti mpya wa SSPRA BW. Athanas Sing'ambi

Aliyekuwa mlezi wa SSPRA MWL.Albert Tibaijuka akitoa busara zake kwa wanachama

viongozi wapya wa sspra katika picha ya pamoja

Baada ya uchaguzi wanachama wakapata picha pamoja na mlezi msaidizi Bw.Frank Katabi

Hosiana Munuo akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya Mhasibu.

Emil Alex akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya Afisa Uhusiano



Athanas Masota akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya Afisa Uhusiano

Joseph Michael akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya katibu  msaidizi

Lodrich Fura akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya katibu msaidizi


Aman Mbwaga Katibu mpya wa SSPRA wakati wa kuomba kura za wanachama

kyando zawadi mtunza fedha mkuu wa SSPRA

Bahati Wilson Mweka hazina Msaidizi wa SSPRA wakati wa kuomba ridhaa ya wanachama kupata nafasi hiyo

Jesse Edwin akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya Afisa Uhusiano msaidizi

Kalumbilo John akiomba kura kutoka kwa wanachama katika nafasi ya Afisa Uhusiano msaidizi


Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Bw.Odilo John akitangaza matokeo ya uchaguzi.




No comments:

Post a Comment