SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Thursday, May 31, 2012

KIKAO CHA MWISHO WA MWAKA KWA WANACHAMA WOTE WA SSPRA.

Wanachama wote wa SSPRA mnaombwa kufika katika kikao cha Mwisho kabisa cha mwaka kitakachofanyika tarehe 2/6/2012 katika darasa la A2-Mwanjonde kuanzia saa 3:00 Asubuhi,Fika bila kukosa mara upatapo taarifa hii basi mtaarifu na Mwanachama mwenzako ili asiweze kupitwa na Kikao hiki Muhimu kabisa cha Mwisho wa Mwaka.

Agenda
  • Kuwasilisha Mipango mkakati kutoka kila Kamati kwa mwaka 2012/2013.
  • Utambulisho wa Wanachama wapya.
  • Kugawa risiti kwa wale waliolipia fomu za kujiunga na SSPRA.
  • Kuwasilisha report ya Mwaka mzima na pia kuonyesha malengo ya mwaka 2012/2013.
  • Na mengineyo
KUFIKA KWAKO NDIO KUFANIKISHA SHUGHULI NZIMA.

EXAMINATION PREPARATION TIPS

For many people, exam time is the most stressful part of the school year. With so much riding on the outcome, there can be a high degree of pressure to perform well. Here are some exam preparation tips to help you excel in school.

Getting Started
The earlier you start, the more time you will have to prepare for the exam. You don't have to wait until exam time approaches; try to set the stage from the beginning of the course by reviewing the material after each class. By starting early and studying on a regular basis, you will have a better opportunity to absorb the information and life will be a lot easier when it's time to put it all together for the exam.

Make sure all of your course material is well organized so you can find and fill any gaps. If you miss any classes, get the notes from your friends right away instead of scrambling at the last minute. Proper organization will help you to get a better picture of the material that has to be covered and improve the flow of the study process.

Creating a Study Plan
As the exam nears, you will need to create a plan to help you study effectively and minimize stress. The first step is to figure out how much time and effort you must dedicate to studying for the exam by asking the following questions:
  • How much material do you need to cover?
  • How difficult is the material?
  • How much time is available?
  • Do you have any other priorities during the study period?
  • What is the format of the exam?
  • How important is the exam?
  • What is your performance target for the exam?
To prepare the study plan, map out all of the material that has to be covered and make a schedule showing what, when and how much you will study each day. If you have kept up with the course work, studying will involve revision of the material that you have already covered. If you are behind in the course, you will have to finish the readings and other uncompleted work before starting the revision (if there isn't enough time to go over everything, you must decide what is most important for the exam).

Wednesday, May 30, 2012

UZINDUZI WA SAUT BUSINESS INCUBATION CENTER

Kesho tarehe 31/05/2012 kuanzia saa 8:00 Mchana- 11:30 katika ukumbi wa M12 katika chuo kikuu cha Mt.Augustino kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kituo cha ujasiliamali kitakachojulikana kwa jina la BUSINESS INCUBATION CENTRE (B.I.C).

Centre hii ni mahususi kabisa katika kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanafunzi wote wa SAUT ambao watakuwa mwaka wa mwisho wa masomo yaani mwaka wa 3 na 4,baada ya kumaliza mitihani yao ya mwisho wa semister watapata fursa ya kuweza kupata mavunzo ya ujasiliamali kwa muda wa miezi 3 BURE kabisa,ambapo chuo kimejitolea kutoa majengo yake,kuleta walimu kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini na nje ya nchi.

Dhumuni la kuanzisha Centre hii ni kuweza kuwasaidia hususan wanafunzi wa SAUT na jamii kwa ujumla njia tofauti tofauti za kuweza kupata fursa za kujiajiri wao wenyewe kwa kuanzisha makampuni yao na pia kuweza kuwapatia mwanga juu ya jinsi gani wanaweza kutumia malighafi zilizopo nchini na kuweza kumiliki njia kuu za uchumi kwa maendeleo ya jamii na pia kwa nchi kwa ujumla badala ya kuwategemea wawekezaji waweze kushikilia njia hizo wakati wanazuoni wapotele hapa nchini huku wakiangaika kwa kutembea na Bahasha mkononi wakiomba ajira katika makampuni na ofsi mbalimbali hapa nchini. 

Center hii itakuwa endelevu,hivyo basi wanafunzi wote  wa kutoka kozi zote za hapa SAUT wanaomaliza masomo yao wanaombwa kuchangamkia nafasi hii ya kipekee kabisa kuweza kutokea hapa SAUT na ndani ya vyuo vya hapa nchini,pia wajasiriamali wa hapa nchini waliofanikiwa watapata fursa ya kuweza kutoa ushuhuda wao ni kwa jinsi gani wameweza kufikia malengo yao waliokuwa wamejiwekea na hatua ambazo wamezitumia mpaka hapa walipofikia,nia ni kuweza kuleta uhalisia halisi kwa wanafunzi hao wakati wa mafunzo. mafunzo haya yatakuwa yamejikita zaidi katika vitendo.

kwa wale wanafunzi watakaoweza kufanya vizuri kwa kuja na michanganuo ya kibiashara (Business plan) zao zitakazokuwa zimeandaliwa vizuri, basi baada ya masomo chuo kitaweza kuwawezesha kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya kuanzisha biashara zao.

Vyombo vya habari,makampuni ya kibiashara mnakaribishwa sana katika uzinduzi huu.
                               Mnakaribishwa nyote. 


Tuesday, May 29, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA USIKU WA MAHAFARI YA SSPRA

Wiki iliyopita siku ya Jumamosi ilifanyika sherehe ya kuwaaga mwaka wa 3 ambao walikuwa ni wanachama wa SSPRA ambapo sherehe hii ya mahafari ilifanyika katika ufukwe wa ziwa Victoria- -Royal Sunset Beach.

Mgeni rasmi katika mahafari hayo alikuwa ni Afsa uhusiano (Public Relations Manager) wa halmashauri ya jiji la mwanza  BW. Joseph Alex Mlinzi. Wanachama 45 walitunukiwa vyeti vyao na wengine 21 kutunukiwa vyeti vya shukrani kwa kuweza kuiongoza vizuri Association mpaka hapa ilipofikia.

Mgeni rasmi .Joseph Mlinzi aliweza kuwapa nasaa wahitimu wote na kuweza kuipongeza  Association kwa kuweza kupiga hatua kubwa sana ukilinganisha na umri wa Association  tangu imeanzishwa...Mgeni rasmi pia aliweza kutoa kiwango cha shilingi Million 1 na laki 2(1,200,000) kwa ajili ya kuweza kuimarisha mfuko wa chama.
Zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo zilichukuliwa wakati wa sherehe hiyo.
Mgeni Rasmi Joseph Mlinzi ambaye ni Meneja Uhusiano wa jiji la Mwanza akiingia ukumbini.

Keki ikibarikiwa na mgeni rasmi.
Viongozi wa SSPRA wakiwa meza kuu
ILIPENDEZAJE
KUTOKA KUSHOTO NI MC, JACQUELINE PATRICK,  CHEBI,NGONYANI NA ATHANASI
Wageni waalikwa wakiwa meza kuu pamoja na mgeni rasmi.
Makamu Mwenyekiti Bw.Chebi akitoa maelezo mbalimbali kwa wageni

Vijana wa Kigomaaa wakitoa show yao ambayo ilivutia wageni na waagwa

Mwl.Denis Mpagaze pia alikuwepo
Wanachama wa mwaka wa Tatu wakitoa burudani kwa mgeni Rasmi

Mwl.Albert Tibaijuka akimpongeza mwenyekiti wa kwanza wa SSPRA Bw.Yusuf Manning




Members walioko mwaka wa pili wakitoa show yao.

Beka,Njumai....wakishine kwa camera

Mwenyekiti Mstaafu Upendo Kessy na Mwenyekiti Msaidizi Medard


Creators .....


aaaah wazamiaji hawakukosekana lol
Glory Kimaro (L) and Njumai Kumba (R)
Francis akipata chakula cha jioni