Taasisi hii inatoa huduma zingine kama ifuatavyo
- Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo.
- Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili.
- Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao.
- Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kisomi zaidi.Hii itafanikiwa kwa kuanzishwa kwa HLSSF ENTREPRENEURSHIP CLUBS kwenye vyuo mbalimbali nchini ambapo wanafunzi wanachama wa HLSSF watakutanishwa pamoja na kuweza kuandaa michanganuo bora.Hii michanganuo itatafutiwa mitaji na HLSSF ili kikundi husika cha wanafunzi waweze kuanzisha na kuendesha rasmi biashara yao.
- Kufanya utafiti juu ya matatizo mbalimbali yanayoikumba sekta ya elimu nchini;pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya uboreshaji wa sera husika.
- Kuendesha workshops,events na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwapatia elimu pana zaidi wafanyabiashara na wanafunzi juu ya maswala ya ujasiriamali, uongozi wa biashara, upatikanaji na uboreshaji wa mitaji,risk management,changamoto za soko huria n.k
- Kutoa ushauri kwa wanafunzi wa sekondari na vyuoni juu ya namna ya kufanya uchaguzi sahihi wa michepuo ya kusoma pamoja na kozi muafaka za kusoma kulingana na changamoto za ajira za sasa.
- Kutoa msaada wa kufanya maombi ya vyuo kwa njia ya mtandao(TCU ONLINE APPLICATIONS) pamoja na kufanya maombi ya mkopo wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) kwa njia ya mtandao (HESLB LOANS ONLINE APPLICATIONS).
GREAT
ReplyDeletewhat are the criteria in order to get education loan
ReplyDelete0656578689
Ata diploma wanapata mkopo???
ReplyDeleteNahitaji mm 0693897658
ReplyDelete