SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Sunday, November 25, 2012

MAONESHO COMMUNITY DAY YAPAMBA JIJI LA MUNGU

Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (SAUT) mwanza kiliazimisha sikukuu ya jamii maarufu kama ''Comunuty day"ambapo idara mbalimbali katika chuo hicho zilifanya maonesho mbalimbali juu ya shughuli zinazo fanyika katika idara hizo.

katika maadhimisho hayo mgeni rasmi Makamu Mkuu wa chuo Padre Dk.Charles Kitima alifungua maonesho hayo na kukagua mabanda mbalimbali ya idara zinazo patikana chuoni hapo.aidha maonesho hayo yalihusisha pia wajasiriamali na makampuni mbalimbali yanyo fanya kazi zake jijini mwanza. Maadhimisho haya yaliandaliwa na Idara ya Mahusiano ya jamii na Matangazo na kuratibiwa na chama cha wanafunzi wanaosoma mahusiano ya jamii na masoko (SSPRA).
Katibu msaidizi wa SSPRA bwana Athanas akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Padre Dk. Charles Kitima katika banda la SSPRA.

Makamu mkuu wa chuo na Waandamizi wake akipata maelezo juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara ya mahusiano ya jamii na Matangazo.



Makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Agustino akiwahutubia wana jumuiya wa SAUT (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Community day




Wanafunzi wanaosoma mahusiano ya jamii na Masoko wakipata maelekezo kutoka kwa mwalimu wao Frank Katabi.

Wanajamii wa SAUT na viunga vyake wakisikiliza hotuba ya mgeni rasimi (hayupo pichani) katika maadhimisho ya community day

Maelezo ya kusisitiza haya kukosekana!!

Tuesday, November 20, 2012

SSPRA WAFANIKISHA UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI JIJINI MWANZA

Leo katika uwanja wa Nyamagana kulifanyika uzinduzi wa kampeni ya "Wazazi nipendeni"ambap wanachama wa SSPRA wameshiriki katika maandalizi na kufanikisha uzinduzi wa kampeni hii wakishirikiana na Afsa Uhusiano wa jiji la Mwanza Bwana Joseph Mlinzi. 

Kampeni hii imezinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa jiji la Mwanza Mhandisi Erasto Ndikilo mnamo saa 4 asubuhi ambapo uzinduzi huo umebeba ujumbe mkuu wa "wazazi nipendeni" (ulinzi mtakao nipa ndio tumaini langu").Pia kampeni hii imeweza kufanikishwa na mashirika mbalimbali kama vile USAID, health Tanzania, Center for communication program, President Malaria initiative,Agakhan Health Centre,na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

Huduma ambazo zilikuwa zikitolewa ni kama vile; kupima afya bure,kupima afya ya mtoto na kupewa dawa bure, pia kupima afya ya mama mjamzito na kuwapa ushauri bure kuhusiana na "mpango binafsi wa kujifungua salama" Pia uzinduzi huu ulisindkizwa na Khalid Mohammed hali maarufu kama TID (Mnyama)kutoka jijini Dar Es salaam pamoja na kundi la uchekeshaji la Futuhi kutoka jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa Erasto Ndikilo akipewa maelekezo kuhusiana na utoaji wa huduma za afya
Wageni rasmi wakiwa meza kuu,mara baada ya ukaguzi wa mabanda ya maonyesho.

Wanachama wa SSPRA wakipanga Fliers na Brochules kwa ajili ya kuwapatia wamama wajawazito.
wanachama wa SSPRA waliofanikisha uzinduzi wa kampeni katika picha ya pamja
wanachama wa SSPRA wakipata maeezo kutoka kwa Afsa Uhusiano wa jiji la Mwanza mwenye koti la kaki

Wanachama wa SSPRA wakitoa maelezo mbalimbali katika kiwanja cha maonyesho






Mkuu wa mkoa kushto akipata maelekezo kutoka banda la Afya ya uzazi 

TID on the stage akiwaburudisha wananchi walifika katika uzinduzi huu
Kikundi cha Ngoma za asili kikimburudisha wanachi waliofia katika uzinduzi.

Kikundi cha Futuhi kikiburudisha wananchi walifika katika uzinduzi












     Afisa uhusiano wa jiji la mwanza bwana Joseph Mlinzi kushoto na Aman E. Mbwaga kulia



Saturday, November 17, 2012

TO NEW SSPRA MEMBERS OF TABORA BRANCH

Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanachama wapya wa SSPRA kutoka tawi la Tabora. Maamuzi mliyochukua ya kujiunga na SSPRA ni sahihi kabisa, Kwa moyo mkunjufu tunawakaribisha sana katika familia kubwa ya kitaaluma yenye mafanikio kila kukicha na mikakati yake ikizidi kufanikiwa kwa ujumla.

Pokeeni salamu nyingi kutoka kwa wanachama wa Mwanza, tunajipanga kuja kuwatembelea katika tawi letu  hilo jipya baada ya kuweka mambo sawa hapa chuoni SAUT-MWANZA.


Kuanzia jumatatu tarehe 19/11/2012 wale wote ambao hawajajiunga mwoneni CR wenu wa PR bwana VIRGIL MBULIGWE atakuwa na Form za kujiunga zitakazokuwa zikipatikana kwa TSH 5000 kwa ajili ya kujiunga,pia kwa wale watakao kuwa wakihitaji  Tshirt za SSPRA zitapatikana kwa Tsh. 15,000 tu.


MWENYEKITI WA SSPRA

NGONYANI CHRISTOPHER

Friday, November 9, 2012

SEMINAR SEMINAR YA INTERNET AND SURFING

WALE MEMBERS WA SSPRA NA WENGINE WENYE MAPENZI MEMA NA ASSOCIATION MNAKUMBUSHWA KWAMBA JUMAPILI SAA 6 MCHANA MPAKA SAA 10 JIONI KUTAKUAWA NA SEMINAR YA INTERNET USE AND SURFING DARASA LA M1,JITAHIDI KUJA NA LAPTOP PAMOJA NA MODEM........FIKA BILA KUKOSA, MPE TAARIFA NA MWINGINE

Thursday, November 1, 2012

MAHAFALI YA 14 CHUO CHA SAUT KUFANYIKA TAREHE 24, NOVEMBER

MAHAFALI YA KUMI NA NNE (14)
Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Mhashamu Baba Askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa anayo furaha kuwatangazia wanafunzi wote
wanaohitimu masomo chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 kwamba,
mahafali ya kumi na nne yatafanyika Jumamosi tarehe 24 Novemba 2012 katika Chuo
Kikuu cha Mtakatifu Agustino kwenye Uwanja wa Raila Odinga kuanzia saa 3.00
asubuhi.
Wahitimu wanaotarajia kushiriki mahafali hayo wanatakiwa kufanya yafuatayo:
1.Kuthibitisha ushiriki wao kwa Wakuu wa Idara kabla ya tarehe 15 Novemba
2012.
2.Wahitimu wanatakiwa kufika Chuoni tarehe 23 Novemba 2012 saa 9 mchana kwa
ajili ya taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa ajili ya
mahafali.

3.Wahitimu wote wanatakiwa kulipa shilingi 50,000 (elfu hamsini tu) kupitia
akaunti ya chuo namba 015101001461 NBC Mwanza. Shilingi 40,000 kwa ajili
ya kuazima joho na shilingi 10,000 kwa ajili ya Cheti cha Taaluma (Academic
Transcript). Wahitimu wanatakiwa kuchukua majoho tarehe 19 mpaka 22
Novemba 2013 kwenye Maktaba ya Chuo cha SAUT.

4.Majoho lazima yarudishwe ndani ya siku mbili baada ya mahafali.Vinginevyo
kutakua na faini ya shilingi 10,000 kwa kila siku itakayozidi.

5.Hosteli za chuo hazina nafasi kwa ajili ya wahitimu hivyo watatakiwa kufanya
mipango ya malazi na usafiri wenyewe.
 
WOTE MNAKARIBISHWA

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania
P .O. Box 307, Mwanza
Tel No: +25528 2552725, Fax +255 28 2550167 Email: dvcaa@yahoo.com