Leo katika uwanja wa Nyamagana kulifanyika uzinduzi wa kampeni ya "Wazazi nipendeni"ambap wanachama wa SSPRA wameshiriki katika maandalizi na kufanikisha uzinduzi wa kampeni hii wakishirikiana na Afsa Uhusiano wa jiji la Mwanza Bwana Joseph Mlinzi.
Kampeni hii imezinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa jiji la Mwanza Mhandisi Erasto Ndikilo mnamo saa 4 asubuhi ambapo uzinduzi huo umebeba ujumbe mkuu wa "wazazi nipendeni" (ulinzi mtakao nipa ndio tumaini langu").Pia kampeni hii imeweza kufanikishwa na mashirika mbalimbali kama vile USAID, health Tanzania, Center for communication program, President Malaria initiative,Agakhan Health Centre,na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.
Huduma ambazo zilikuwa zikitolewa ni kama vile; kupima afya bure,kupima afya ya mtoto na kupewa dawa bure, pia kupima afya ya mama mjamzito na kuwapa ushauri bure kuhusiana na "mpango binafsi wa kujifungua salama"
Pia uzinduzi huu ulisindkizwa na Khalid Mohammed hali maarufu kama TID (Mnyama)kutoka jijini Dar Es salaam pamoja na kundi la uchekeshaji la Futuhi kutoka jijini Mwanza.
|
Mkuu wa mkoa Erasto Ndikilo akipewa maelekezo kuhusiana na utoaji wa huduma za afya |
|
Wageni rasmi wakiwa meza kuu,mara baada ya ukaguzi wa mabanda ya maonyesho. |
|
Wanachama wa SSPRA wakipanga Fliers na Brochules kwa ajili ya kuwapatia wamama wajawazito. |
|
wanachama wa SSPRA waliofanikisha uzinduzi wa kampeni katika picha ya pamja |
|
wanachama wa SSPRA wakipata maeezo kutoka kwa Afsa Uhusiano wa jiji la Mwanza mwenye koti la kaki |
|
Wanachama wa SSPRA wakitoa maelezo mbalimbali katika kiwanja cha maonyesho |
|
Mkuu wa mkoa kushto akipata maelekezo kutoka banda la Afya ya uzazi |
|
TID on the stage akiwaburudisha wananchi walifika katika uzinduzi huu |
|
Kikundi cha Ngoma za asili kikimburudisha wanachi waliofia katika uzinduzi. |
|
Kikundi cha Futuhi kikiburudisha wananchi walifika katika uzinduzi |
Afisa uhusiano wa jiji la mwanza bwana Joseph Mlinzi kushoto na Aman E. Mbwaga kulia
No comments:
Post a Comment