SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Thursday, November 1, 2012

MAHAFALI YA 14 CHUO CHA SAUT KUFANYIKA TAREHE 24, NOVEMBER

MAHAFALI YA KUMI NA NNE (14)
Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Mhashamu Baba Askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa anayo furaha kuwatangazia wanafunzi wote
wanaohitimu masomo chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 kwamba,
mahafali ya kumi na nne yatafanyika Jumamosi tarehe 24 Novemba 2012 katika Chuo
Kikuu cha Mtakatifu Agustino kwenye Uwanja wa Raila Odinga kuanzia saa 3.00
asubuhi.
Wahitimu wanaotarajia kushiriki mahafali hayo wanatakiwa kufanya yafuatayo:
1.Kuthibitisha ushiriki wao kwa Wakuu wa Idara kabla ya tarehe 15 Novemba
2012.
2.Wahitimu wanatakiwa kufika Chuoni tarehe 23 Novemba 2012 saa 9 mchana kwa
ajili ya taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa ajili ya
mahafali.

3.Wahitimu wote wanatakiwa kulipa shilingi 50,000 (elfu hamsini tu) kupitia
akaunti ya chuo namba 015101001461 NBC Mwanza. Shilingi 40,000 kwa ajili
ya kuazima joho na shilingi 10,000 kwa ajili ya Cheti cha Taaluma (Academic
Transcript). Wahitimu wanatakiwa kuchukua majoho tarehe 19 mpaka 22
Novemba 2013 kwenye Maktaba ya Chuo cha SAUT.

4.Majoho lazima yarudishwe ndani ya siku mbili baada ya mahafali.Vinginevyo
kutakua na faini ya shilingi 10,000 kwa kila siku itakayozidi.

5.Hosteli za chuo hazina nafasi kwa ajili ya wahitimu hivyo watatakiwa kufanya
mipango ya malazi na usafiri wenyewe.
 
WOTE MNAKARIBISHWA

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania
P .O. Box 307, Mwanza
Tel No: +25528 2552725, Fax +255 28 2550167 Email: dvcaa@yahoo.com

No comments:

Post a Comment