SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Friday, February 17, 2012

SSPRA WAFANYA ZIARA KATIKA KAMPUNI YA NYANZA BOTTLING

Wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Augustino (Mwanza )wanaosoma shahada ya Uhusiano wa Umma na Masoko ,leo wamefanya ziara ya mafunzo katika kampuni ya Cocacola (Nyanza Bottling Company Limited).Ili kupata mafunzo mbalimbali kuhusiana namna uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo unavyofanyika.

Ziara hiyo iliandaliwa na chama cha wanafunzi wasomao uhusiano wa Umma SSPRA (SAUT STUDENT’S PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION)iliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya vitendo kwa wanachama wao hususani katika uhusiano wa umma na masoko yanayofanya na kampuni hiyo.

Aidha wakati wa mafunzo hayo maswali kadhaa yaliulizwa hasa pale wanafunzi walipotaka kujua wapi malighafi zinatolewa kwaajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo,kufuatia swali hilo mwelimishaji alibainisha kuwa malighafi nyingi zitumikazo katika uzalishaji kama vile sukari ,uzalishaji wa chupa hutoka chi za nje kama vile Brazil, Saudi Arabia, Afrika kusini sababu zilizotolewa na mwelimishaji bwana Mlekwa Pius aliyoko Sugar Store kuhisiana na uagizaji wa sukari kutoka nchi za nje alisema kuwa makampuni yanayohusika na uzalishaji wa sukari hayakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya uzalishaji wa soda hivyo inasababisha serikali kukosa mapato.

Uongozi wa SSPRA unapenda kutoa shukrani zake kwa Uongozi wa Kampuni ya Nyanza Bottling kwa kuweza kufanikisha ziara yao na kwa wafanyakazi wao ambao wameweza kutoa mafunzo kwa wanachama wa SSPRA bila kuchoka pale walipokuwa wanaulizwa maswali.

Lango kuu









Mashine inayotumika kutengenezea chupa za plastic za soda

chupa zinapita kwenye mitambo kwa ajili ya kusafishwa





ndani ya chumba cha usafishaji chupa
baada ya kuangalia uzalishaji wa chupa wanachama wakachukua japo picha ya ukumbusho.
Anthonius pamoja na Francis wakishangaa hatua ya kwanza ya chupa ya plastic kabla haijaingizwa kwenye mashine kujazwa upepo
Hizi ndo chupa za plastic kabla hazijawekwa kwenye mashine kwa hatua ya mwisho kuwekewa upepo iweze kupanuka kwa ajili ya kuwekewa soda
Ndani ya chumba cha utengenezaji wa maumbo mbalimbali ya chupa
Members wakiwa nje wakisubili kuingia ndani.


Anajulikana kwa jina la bwana Dotto Andrew ambaye yuko stoo ya sukari,alikuwa anatoa maelezo mbalimbali juu ya uchanganyaji wa sukari na kiwango kinachohitajika kwa kila soda

Nyanja and Ally
Nyanja and Daniel
Anthonius and Daniel

Mwenyekiti wa SSPRA upendo Kessy akiwa na Francis Moses mwenyekiti wa kamati ya Uhusiano wa vyombo vya habari na machapisho



Nyanja and Zawadi
Jacqueline Patrick Katibu msaidizi wa SSPRA
Erick Charles na Magafu



No comments:

Post a Comment