SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Saturday, June 22, 2013

TANGAZO KWA WANACHAMA WOTE WA SSPRA

Wale wote ambao wanapenda kushiriki katika safari yetu ya kimasomo Nairobi_Kenya katika mwaka wa masomo ujao(Mwezi wa tisa),Mnakumbushwa Kuchukua Fomu za kukusaidia wewe Mwanachama wa Sspra Kuchangisha Fedha ya michango kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo. 
      Fomu zimeanza kutolewa leo 20/06/2013 Mpaka 2/07/2013.
    
FOMU ZINAPATIKANA KWA_:
    KATIBU MKUU WA SSPRA (+2557650558711/+255714197141
                                            Email;prof.mbwaga@gmail.com
  
MWENYEKITI WA SSPRA,(+255755154215
                                   
    WAHI MAPEMA FOMU NI CHACHE!

Saturday, June 8, 2013

SSPRA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO WAANDAA SHEREHE YA KUMUAGA PADRI DOKTA CHARLES KITIMA JANA KATIKA UWANJA WA RAILA ODINGA.




Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mt.Augustino Mwanza(SAUT) Mh.Padri Dokta Charles Kitima leo amewaaga wanafunzi na jumuiya yote ya mtakatifu augustino katika kiwanja cha raila odinga na kumkaribisha Makamu Mkuu Mpya Padri Pius Mgeni kuwa ndiye makamu mkuu wa chuo kwa sasa.

Akizungumza katika sherehe hiyo ya kumuaga padri charles kitima awewataka wasomi wote wa vyuo vikuu na viongozi wote kuiga mfumo wa hayati Mwalimu J.K Nyerere ambao aliutumia katika kuiongoza Tanganyika na kuwa mstari wa mbele katika kutetea rasimali za wazawa ambazo utoroshwa kwenda nje kwa njia za panya.

Aidha,Amewataka vijana kuendelea kusoma kazi mbalimbali ambazo Hayati Mwalimu JK Nyerere katika uhai wake aliwahi kuziandika kwa ajili ya watanzania,kama marejeo ya kuondokana na matatizo yanayoikabili la tanzania kwa sasa.

 Katika sherehe hiyo ya kumuaga iliendana sambamba na kikizinduua kitabu kipya kilichoandikwa na Boniphace Pesambili Mgeta ambaye ni mwanafunzi katika shahada ya mwasiliano ya umma(Bachelor of Arts in Mass Communications) katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza.Pia amempongeza boniphace kwa kuandika hicho kitabu na kutaka aendeleze weledi katika kuandika kazi ambazo zinatetea haki za watanzania.

Padri charles kitima ametoa zawadi ya kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha mtakatifu augustino kwa kuwanunulia nakala 300 ya vitabu vilivyoandikwa na Bw. Boniphace Mgeta

Kitabu hicho kimeandikwa kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wailosoma katika chuo hicho katika kafuta suluhisho la matatizo mbalimbali ambayo yanawakabiri watanzania kwa sasa.

Zoezi hilo la uzinduzi wa kitabu lilisindikizwa na wakuu wa idara mbalimbali,Idara ya mawasiliano ya umma,Mkuu wa Idara ya sheria,na Mkuu wa idara ya Mahusiano ya jamii na matangazo.