Saut Students Public Relations Association (SSPRA) Ilifanikisha safari yake Tarehe 20/11/2013 hadi Tarehe 23/11/2012. Safari hiyo ni moja ya malengo Makuu iliyokuwa imejipangia mwaka huu, na sasa yametimia hii ni kutokana na ushirkiano mzuri baina ya viongozi na wanachama wake na mahusiano mazuri na vyuo vingine ambapo safari hii ilifanikiwa kwa kuunganisha na wanafunzi wa mahusiano ya umma na masoko kutka chuo kikuu kishirki cha Mt Agustino Tawi la TABORA(AMUCTA)
Safari ilianza siku ya JumatanoTarehe 20/11/2013, kutoka chuo kikuu cha Mt.Agustino Mwanza. Mnamo saa 5:00 asubuhi tuliwasili Mpakani mwa Tanzania Na Kenya mpaka ujulikanao kama SAILARI ambapo hapo tulipigiwa mihuri pasipoti zetu za kusafiria na kupata insuarance ya Basi letu la chuo, pia tulitumia muda huo kubadilisha fedha zetu na kupata fedha za kenya. zoezi lote lilichukua muda wa masaa matatu. Mnamo saa 8:00 mchana tulianza safaari rasimi ya kuelekea ktk jiji la Nairobi na tuliwasili jijini Nairobi mida ya saa 4 usiku.
Tarehe 21/11/2013 ,Tuliamka na kuanza shughuli ya kutembelea Maeneo Muhimu ya jiji la Nairobi na Baadhi ya maeneo tuliyotembelea ni pamoja na sehemu ya Mikutano ya Kimataifa. KENYA INTERNATIONAL CONVETION CENTER (KICC) Pia hapo tulitembeleea Maonesho Makubwa yaliyojulikana Kama KENYA INDUSTRIALIZATION ambapo walikuwa wakionesha na kuhimiza wananchi wao kununua na kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini mwao.
Hapa tumejifunza nasi umuhimu wa kutangaza bidhaa zetu wenyewe zinazozalishwa hapa nchini ili kuvipa nguvu viwanda vyetu vidogo na hii inapelekea kuinua uchumi wa nchi yetu ya Tanzania kwa kiasi kikubwa pia itaondoa dhana ya utegemezi.
Pia tulitembelea Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Jommo Kenyata, Viwanja vya uhuru Park,Ofisi ya Rais wa Kenya Ofisi ya makamu wa Rais wa kenya, na Ubalozi wa Markani uliolipuliwa na magaidi, nk,
Tarehe 22/11/2013 kuanzia saa 02:30 asubuhi Tulikutana na wanafunzi wenzetu wa chuo kikuu Nairobi Pale chuoni kwao. na mara baada ya kuwasili chuni hapo tulipokelewa vizuri sana na ndipo wanafunzi wa SAUT, Tulianza kugawa vipeperushi ambavyo vimebeba jumbe mbalimbali zinazokihusu chuo chetu.
Lengo lilikuwa ni kukitangaza chuo chetu zaidi na zoezi lile lilifanikiwa kwa asilimia kubwa.Mara baada ya hapo Tulianza Kongamano la kielimu, ambalo lilihusu zaidi masuala ya umuhimu wa mameneja mahusiano, mwasiliano na waaandishi wa habari..Ambapo wataalamu mbalimbali walialikwa na wakawsilisha pepa zao kwa kiwango cha hali ya juu, pia kulikuwa na kipindi cha maswali na majibu ambapo wataalamu hao waliweza kuyajibu kwa ufasaa zaidi wakiongozwa na Profes kutoka chuo kikuu cha Moi nchini Kenya. Baadhi ya wataalamu hao, wasifu wao na mada walizowasilisha ni hizi zifuatazo.
1. BY: PROF. OKUMU-BIGAMBO, W. (PHD, MA, PGDE, and BA)
CONSULTANT/TRAINER OF TRAINERS: COMMUNICATION AND PUBLIC RELATIONS; DEPT OF COMMUNICATION STUDIES; SCHOOL OF HUMAN RESOURCE DEVELOPMENT; MOI UNIVERSITY;
P.O.BOX 8630-30100 ELDORET, KENYA; TEL. 0722356211;
He present about PUBLIC RELATIONS: THE ART AND THE PROFESSION
2. David Ohito
Worked at Standard Group (standard Digital News –kenya)
Past worked at KTN TV, He studied Media and Politics at MOI,POYNTER INSITUTE and Past at Nairobi University.
He present about Media in Digital Age and Media convergence etc.
3. Jay Bonyo
Worked at Nation Media Group as a Chief Editor
He present about the importance of Networking as a communicators personnel
4.Shisiha Wasilwa
Sub Editor, Royal Media Service, anchor news reporter and also stories editor Before joining Royal Media he was Worked at Kenya Broadcasting Corporation
(KBC)
He present about the role of Swahili Language In the media house of Kenya
Kufikia saa 09:30 alasiri Tulimaliza kongamano letu na wanafunzi wenzetu ambao wako chini ya idara ya Mawasiliano ya umma. ( School of Journalism and Mass comminication under the falcuty of Humanities and social sciences) Na ndipo tulianza safari yetu ya kurejea Nchini Kwetu Tanzania. Tulianza safari mapema ili kuwahi kutembelea Bonde la Ufa lililopo nchini Kenya.(RIFTVALLEY) na kwa kweli linvutia sana kwa kuliangalia tu. Baada ya kumaliza kutembelea Bonde la ufa ndipo tulipoaanza safari rasmi ya kurudi.
Tarehe 23/11/2013siku ya jumamosi Tuliwasili nchini Tanzania ktk Jiji la Mwanza Mnamo saa 7:00 mchana pale Lavour center ambapo wote tulimshukuru mungu kwa ajili ya safari yetu kwa kwenda salama na kurudi salama safari ilikua nzuri sana na yenye mafankio makubwa na kila aliyeenda aliifurahia na kumshukuru mungu kwa kuifanikisha.
Mwisho tunamashukuru sana Mungu wetu alie Hai kwa kutuwezesha kutimiza ndoto zetu za chama kwa lengo la kujifunza zaidi.
Pia shukrani zetu za dhati ziwafikie Utawala wetu Wa Chuo kikuu cha Mt AgustinoTanzania, VC, PRINCIPAL AMUCTA, DVCAA, BURSER, PRO, DEAN OF FALCUTY OF SOCIAL SCIENCES & COMMUNICATION, DEAN OF STUDENTS, HOD, PATRON, Mr Lila Say Mandu & Mr Ikachoi Denis (Wahadhiri wa chuo kikuu SAUT Idara ya mawasiliano ya umma na Matangazo) Pia wanachama wa SSPRA kutoka SAUT TABORA chini ya Uongozi makini wa Dada Patrica Mwumi Amabaye ndio Mwanyekiti wa Tabora Pia Viongozi wa SSPRA Mwanza Kwa ushirikiano mzuri na Wanachama wote kwa kufanikisha adhma yetu.
"Mungu ibariki Tanzania" " Mungu ibariki SAUT", "Mungu ibariki SSPRA".
SSPRA- Join our Professional Hands
Imeandaliwa na :
Mbwaga Aman E
KATIBU MKUU (SSPRA)
Mob: +255765058711, Email: prof. mbwaga@gmail.com
PICHA NA MATUKIO YALIYOJILI KATIKA SAFARI YETU YA NAIROBI
|
Wanachama wa SSPRA Wakiwa Eneo la Mikutano ya kimataifa KICC Mara baada ya kumaliza Maonesho. |
|
Viongozi Wa SSPRA Wakiwa na Rais wa PRSK Tawi la chuo kikuu Nairobi Bwana Robert Kenyando wa pili kutoka kulia |
|
Baadhi ya kina dada wa SSPRA Mara Baada Ya Kuwasili Chuoni Nairobi
|
|
Wanachama wa SSPRA Wakiwa ktk basi la chuo Kuelekea Nairobi. |
|
Katibu mkuu Aman Mbwaga Kushoto Na Kulia Ni Katibu msaidizi wa SSPRA Mr Rodriche |
|
Wanachama wa SSPRA wakitembelea mabanda ya maonesho jijini Nairobi. |
|
Mr Thomas Laurent Katibu wa Kamati ya Debate and Forum |
|
Baadhi ya Majengo ya Chuo kikuu Nairobi nchini Kenya. |
|
Wanachama wa SSPRA Wakitembelea moja ya SUPERMARKET Kubwa jijini Nairobi. |
|
Mwl. Lila Say Mandu ( mkuu wa msafara) akitoa maelekezo ktk viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi
|
|
Moja ya usafiri Maarufu jijini Nairobi Ujulikanao kama Matatu .
|
|
Aman Mbwaga akiwa na Dereva Mr Sylivester |
|
Moja ya usafiri Maarufu jijini Nairobi Ujulikanao kama Matatu . |
|
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Kenya.
|
Mr Jay Bonyo chief Editor Akitoa mada kwa Wanafunzi Wa SAUT Na wa Chuo kikuu Nairobi |
|
|
Mwenyekiti wa SSPRA Singambi Athanas. akiwa ktk chuo kikuu Nairobi. |
|
Wanachama wa SSPRA wakiwa katika Bonde la Ufa la Kenya. |
|
PRO wa SSPRA Kushoto Katikati ni Mwenyekiti a SSAPRA SAUT-TABORA |
|
Baadhi ya wanachama wa SSPRA wakitoka ktk ukumbi wa kimataifa KICC. |
|
Hii ni Menyu ya Chakula na Bei zake ktk cafteria ya chuo kikuu Nairobi |
|
Viongozi wa SSPRA Wakiwa tayari kwa safari ya kurejea Tz. |
|
Esther Venancy Mwenyekiti wa Fundrising akiwasili chuoni Nairobi |
|
Mti Maarufu Uliopandwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere ktk chuo kikuu cha Nairobi |
|
Katibu mkuu SSPRA, Bwana Aman Mbwga akiongea na baadhi ya wanafunzi wanaosoma Masters Naiobi Waliotokea SAUT |
|
Naibu katibu msaidizi wa SSPRA Akibadilishana mawazo na wanafunzi wa chuo kikuu Nairobi. pia akiwagawa vipeperushi vinavyohusiana na chuo kikuu SAUT. |
|
PROF. OKUMU-BIGAMBO Kutoka chuo kikuu cha Moi akijibu baadhi ya maswali ya wanafunzi. |
Tunaomba Radhi kwa baadhi ya Picha kutoonekana vizuri.
Be blessed!