Katika kikao kilichofanyika jumamosi cha wanachama wote mwanjonde (B3) wanachama hao wote kwa pamoja wameazimia kufanya mahafali ya kuwaaga mwaka wa mwisho kama ilivyo andikwa katika kichwa cha habari hapo juu.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa sspra Athanas Sing'ambi amethibitisha hilo na kuwataka wanachama wote kushirikiana kwa pamoja kwa wale wa mwaka wa kwanza hadi wa mwisho ili kufanikisha tukio hilo la kuwaaga wanachama wenzetu wa mwaka wa mwisho.
Sherehe hiyo itafanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa ROYAL SUNSET BEACH iliyoko katika kijiji cha luchelele hivyo basi ili kufanikisha mahafali hayo wanachama wote mnaombwa kuendelea kutoa michango yenu kwa viongozi ambao mmekwisha elekezwa kwenda kutoa hiyo michango ya mafahali.
Mwenyekiti pia amewataka wanachama wote hasa wale wanaobaki kuendelea kufika katika vikao vyote vitakao kuwa vikiitishwa na wale ambao watakuwa hawaji katika vikao hivyo basi hatua kali zitachukukiwa na kamati husika, kwa wale ambao watakukuwa wanashindwa kuja katika vikao hivyo basi wanaombwa wawe wanatoa taarifa kwa viongozi wapya wa sspa ili kuepuka usumbufu kwa hapo baadaye.
SSPRA INAWATAKIA WANACHAMA WOTE MAANDALIZI MEMA YA MAHAFALI YA KUWAAGA MWAKA WA TATU NA KAMATI HUSIKA YA MAHAFALI IFANYE JITIHADA ZOTE ILI KUFANIKISHA MALENGO YALIYO AZIMIWA NA WANACHAMA WOTE KWA PAMOJA!
No comments:
Post a Comment