Kesho
tarehe 31/05/2012 kuanzia saa 8:00 Mchana- 11:30 katika ukumbi wa M12
katika chuo kikuu cha Mt.Augustino kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kituo
cha ujasiliamali kitakachojulikana kwa jina la BUSINESS INCUBATION
CENTRE (B.I.C).
Centre
hii ni mahususi kabisa katika kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanafunzi
wote wa SAUT ambao watakuwa mwaka wa mwisho wa masomo yaani mwaka wa 3
na 4,baada ya kumaliza mitihani yao ya mwisho wa semister watapata
fursa ya kuweza kupata mavunzo ya ujasiliamali kwa muda wa miezi 3 BURE kabisa,ambapo chuo kimejitolea kutoa majengo yake,kuleta walimu kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini na nje ya nchi.
Dhumuni
la kuanzisha Centre hii ni kuweza kuwasaidia hususan wanafunzi
wa SAUT na jamii kwa ujumla njia tofauti tofauti za kuweza kupata fursa
za kujiajiri wao
wenyewe kwa kuanzisha makampuni yao na pia kuweza kuwapatia mwanga juu
ya
jinsi gani wanaweza kutumia malighafi zilizopo nchini na kuweza
kumiliki njia kuu za uchumi kwa maendeleo ya jamii na pia kwa nchi kwa
ujumla badala ya kuwategemea wawekezaji waweze kushikilia njia hizo
wakati wanazuoni wapotele hapa nchini huku wakiangaika kwa kutembea na
Bahasha mkononi wakiomba ajira katika makampuni na ofsi mbalimbali hapa
nchini.
Center
hii itakuwa endelevu,hivyo basi wanafunzi wote wa kutoka kozi zote za
hapa SAUT wanaomaliza masomo yao wanaombwa kuchangamkia nafasi hii ya
kipekee kabisa kuweza kutokea hapa SAUT na ndani ya vyuo vya hapa
nchini,pia wajasiriamali wa hapa nchini waliofanikiwa watapata fursa ya
kuweza kutoa ushuhuda wao ni kwa jinsi gani wameweza kufikia malengo
yao waliokuwa wamejiwekea na hatua ambazo wamezitumia mpaka hapa
walipofikia,nia ni kuweza kuleta uhalisia halisi kwa wanafunzi hao
wakati wa mafunzo. mafunzo haya yatakuwa yamejikita zaidi katika
vitendo.
kwa wale wanafunzi watakaoweza kufanya vizuri kwa kuja
na michanganuo ya kibiashara (Business plan) zao zitakazokuwa zimeandaliwa vizuri, basi baada ya
masomo chuo kitaweza kuwawezesha kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya
kuanzisha biashara zao.
Vyombo vya habari,makampuni ya kibiashara mnakaribishwa sana katika uzinduzi huu.
Mnakaribishwa nyote.
No comments:
Post a Comment