Wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Augustino (Mwanza )wanaosoma shahada ya Uhusiano wa Umma na Masoko ,leo wamefanya ziara ya mafunzo katika kampuni ya Cocacola (Nyanza Bottling Company Limited).Ili kupata mafunzo mbalimbali kuhusiana namna uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo unavyofanyika.
Ziara hiyo iliandaliwa na chama cha wanafunzi wasomao uhusiano wa Umma SSPRA (SAUT STUDENT’S PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION)iliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya vitendo kwa wanachama wao hususani katika uhusiano wa umma na masoko yanayofanya na kampuni hiyo.
Aidha wakati wa mafunzo hayo maswali kadhaa yaliulizwa hasa pale wanafunzi walipotaka kujua wapi malighafi zinatolewa kwaajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo,kufuatia swali hilo mwelimishaji alibainisha kuwa malighafi nyingi zitumikazo katika uzalishaji kama vile sukari ,uzalishaji wa chupa hutoka chi za nje kama vile Brazil, Saudi Arabia, Afrika kusini sababu zilizotolewa na mwelimishaji bwana Mlekwa Pius aliyoko Sugar Store kuhisiana na uagizaji wa sukari kutoka nchi za nje alisema kuwa makampuni yanayohusika na uzalishaji wa sukari hayakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya uzalishaji wa soda hivyo inasababisha serikali kukosa mapato.
Uongozi wa SSPRA unapenda kutoa shukrani zake kwa Uongozi wa Kampuni ya Nyanza Bottling kwa kuweza kufanikisha ziara yao na kwa wafanyakazi wao ambao wameweza kutoa mafunzo kwa wanachama wa SSPRA bila kuchoka pale walipokuwa wanaulizwa maswali.
Mashine inayotumika kutengenezea chupa za plastic za soda
chupa zinapita kwenye mitambo kwa ajili ya kusafishwa
ndani ya chumba cha usafishaji chupa
baada ya kuangalia uzalishaji wa chupa wanachama wakachukua japo picha ya ukumbusho.
Members wakiwa nje wakisubili kuingia ndani.
Nyanja and Ally
Nyanja and Daniel
Anthonius and Daniel
Nyanja and Zawadi
Jacqueline Patrick Katibu msaidizi wa SSPRA
Erick Charles na Magafu
No comments:
Post a Comment