Kutoka chuo kikuu cha Mt.Augustine,leo limefanyika collage baraza ambalo limewakutanisha Makamu mkuu wa chuo (VC Charles Kitima), Dean Of Students (mama Nasania), Corporate counsel, serikali ya wanafunzi (SAUTSO) pamoja na wanafunzi wa chuo cha SAUT kwa pamoja kwa ajili ya kuzungumzia kero mbalimbali ambazo zinawakabili wanafunzi wawapo ndani na nje ya chuo,mengi yamesemwa na wanafunzi na kutolewa ufafanuzi na Makamu mkuu wa chuo.
Yafuatayo ndio yaliweza kutolewa ufafafanuzi na makamu mkuu wa chuo.
1. Swala la ulinzi hafifu ndani na nje ya chuo,Makamu mkuu wa chuo ametoa ufafanuzi kuwa swala hilo limeshafika chini ya uongozi wake na wanalifanyia kazi hasa kwa kuboresha kampuni ya ulinzi iliyopo chuoni kwa kuongeza idadi ya walinzi wengi wa kufanya patrol kila wakati,pia swala la kujenga kituo cha polisi eneo la Nsumba amesema kuwa “Hakuna haja ya kujenga kituo cha polisi Nsumba kwa sababu polisi wanawekewa lita za mafuta kwenye gari zao kwa ajili ya kufanya patrol eneo lote la chuo hivyo hata kikijengwa bado itawabidi wafanye patrol tu eneo zima hivyo kituo kilichopo Nyegezi kinatosha.”
2. Ulipaji wa faini ya shilingi laki moja, VC Kitima amesema kuwa wale wote wanaochelewesha ulipaji wa ada bila sababu za msingi basi lazima faini hiyo Wailipe ametoa msimamo wake kwa kusema kuwa “hatakuwa na msamaha kabisa kuhusu faini hiyo”,akaendelea kutoa ufafanuzi kuwa kwa wanafunzi ambao watakuwa na matatizo yoyote kuhusu ada basi wafike katika ofsi ya DVCAF - father Mwanjonde kwani ndiye amepewa mamlaka yote yanayohusiana na swala la ada na mambo mengine yote yanayohusiana na fedha.
3. Tatizo la lugha chafu inayotolewa na baadhi ya wafanyakazi wa chuo,VC Kitima amesema swala hilo atalifuatilia kwa ukaribu kabisa na kwa wote watakaobainika kufanya hivyo basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kusimamishwa kazi,wanafunzi wamekuwa wakilalamikia baadhi ya ofsi za chuo ambapo wamekuwa wakikutana na lugha zizizolizisha na saa zingine kuambulia matusi,na ofsi hizo zilianikwa wazi kuwa ni kwa mkuu wa idara ya Elimu (Mabere),ofsi wa wahasibu wa chuo, ofsi inayohusika na mikopo ya wanafunzi.
4. Tatizo la miundo mbinu kwa wanafunzi wenye ulemavu, chuo kimeonekana kutokuwa na miundombinu ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kupanda ngazi wakati wa vipindi au Makitaba kwenye magorofa makamu katolea ufafanuzi kuwa majengo yote hayo yanasehemu maalum kabisa kwa ajili ya kuweka lift zitakazo ondoa tatizo hilo lakini bado imeshindikana kwa sasa kwa sababu ya tatizo la uchumi ambalo linaikabili nchi na hata chuo chenyewe akaendelea ksema kuwa gharama ya kununua lift moja ni sawa na kujenga darasa moja kama M13.
5. Uwepo wa kozi nyingi kwa muhula mmoja, wanafunzi wamekuwa wakilalamika sana juu ya kuwepo masomo mengi mpaka kufikia kozi 12 kwa semester,VC Kitima kasema kuwa hii ni private university ina sheria zake za kiutendaji hivyo kozi hizo haziwezi kutolewa na nia siyo kumuumiza mwanafunzi bali ni kumweka katika mazingira mazuri ya kupata maarifa ya kutosha ili aweze kuendana na soko la ajira na kuweza kumweka mwanafunzi wa SAUT kuwa tofauti na wanafunzi wa vyuo vingine.
6. Tatizo la mikopo ya wanafunzi, wanafunzi wamekuwa wakilalamika juu ya ucheleweshwaji wa mikopo yao na wengine majina yao kutokutolewa kwa wakati,Makamu mkuu kasema kuwa swala la mikopo ni mkataba kati ya bodi na mwanafunzi husika na sio SAUT lakini wao wanaweza kusaidia pindi panapobidi,akafafanua kuwa mpaka sasa hivi bodi bado hawajotoa fedha za ada kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo hiyo,hivyo kuna uwezekano wanafunzi wasifanye mitihani ya mwisho wa semester ya kwanza.
7. Tatizo la uhaba wa computer makitaba na internet, VC Fr. Kitima ameweka bayana kuwa swala hilo linafatiliwa kwa ukaribu kabisa na tayari wamefunga mkonge wa Taifa wa Internet na hivi punde utaanza kutumika hapa chuoni na pia kawapa ushauri wanafunzi wajitahidi wanunue laptop ili waweze kwendana na mabadiliko ya sayansi na technolojia.
Mambo mengi yamezungumzwa pia mafanikio yamewekwa bayana mfano chuo kimeweza kuajiri wahadhili mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa nia moja tu ya kuweza kuimarisha na kutoa elimu bora,pia mkuu kasema yuko tayari kuajiri mhadhili yoyote kwa bei yoyote ili kuweza kuboresha elimu.VC kapongeza pia serikali ya wanafunzi kwa kuwajibika vizuri na pia kwa kushirikiana na uongozi wa chuo, Makamu pia katoa nasaha zake kwa wanafunzi wote hasa wasichana kujiepusha na kwenda night clubs kwani hazina umuhimu wowote bali zinaharibu performance katika taaluma.
No comments:
Post a Comment