SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Saturday, December 15, 2012

SSPRA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA STAREHE, JIJINI MWANZA


Wanachama wa SSPRA leo tarehe 15/12/2012 wametembelea na kutoa misaada ya chakula na malazi kwa ajili ya kuwasaidia watoto walioko kituo cha STAREHE CHILDREN'S HOME kilichopo eneo la Nyegezi jijini Mwanza, wanachama wa SSPRA wametoa msaada huo kwa watoto yatima katika kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka  X-MASS na mwaka mpya ikiwa ni mojawapo ya majukumu ya kuisaidia jamii inayotuzunguka (CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY).

Kituo hiki kinahudumia watoto yatima,waliotelekezwa kuanzia umri wa miaka 0-5, watoto hawa huletwa kituoni hapo kutoka Ustawi wa jamii na sio kwamba wao ndio huwatafuta watoto hao. BW.GETSON EZEKIEL ambaye ni Daktari wa watoto hao walioko kituoni hapo.

Baadhi ya watoto walioko kituoni hapo wakipokea msaada kutoka SSPRA


Joseph Michael akimkabidhi Dr. Ezekiel  kadi ya X-MASS na Mwaka Mpya.


Watoto waliopo kituoni hapo wa


Muddy akikabidhi naye zawadi yake kwa mtoto



wanachama wakifika kituoni hapo muda wa asubuhi.



wanachama wakifanya usafi.........

Aman Mbwaga akifanya naye usafiiiiii



wanachama wakiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa kituo

Kutoka kushoto ni mwenyeketi wa SSPRA Bw.Ngonyani Christopher, Dr Getson Ezekiel,na Afsa Ustawi wa jamii kituoni hapo.


Waachama wakibadilishana mawazo

PR 3 Members wa SSPRA



Sunday, November 25, 2012

MAONESHO COMMUNITY DAY YAPAMBA JIJI LA MUNGU

Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (SAUT) mwanza kiliazimisha sikukuu ya jamii maarufu kama ''Comunuty day"ambapo idara mbalimbali katika chuo hicho zilifanya maonesho mbalimbali juu ya shughuli zinazo fanyika katika idara hizo.

katika maadhimisho hayo mgeni rasmi Makamu Mkuu wa chuo Padre Dk.Charles Kitima alifungua maonesho hayo na kukagua mabanda mbalimbali ya idara zinazo patikana chuoni hapo.aidha maonesho hayo yalihusisha pia wajasiriamali na makampuni mbalimbali yanyo fanya kazi zake jijini mwanza. Maadhimisho haya yaliandaliwa na Idara ya Mahusiano ya jamii na Matangazo na kuratibiwa na chama cha wanafunzi wanaosoma mahusiano ya jamii na masoko (SSPRA).
Katibu msaidizi wa SSPRA bwana Athanas akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Padre Dk. Charles Kitima katika banda la SSPRA.

Makamu mkuu wa chuo na Waandamizi wake akipata maelezo juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara ya mahusiano ya jamii na Matangazo.



Makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Agustino akiwahutubia wana jumuiya wa SAUT (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Community day




Wanafunzi wanaosoma mahusiano ya jamii na Masoko wakipata maelekezo kutoka kwa mwalimu wao Frank Katabi.

Wanajamii wa SAUT na viunga vyake wakisikiliza hotuba ya mgeni rasimi (hayupo pichani) katika maadhimisho ya community day

Maelezo ya kusisitiza haya kukosekana!!

Tuesday, November 20, 2012

SSPRA WAFANIKISHA UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI JIJINI MWANZA

Leo katika uwanja wa Nyamagana kulifanyika uzinduzi wa kampeni ya "Wazazi nipendeni"ambap wanachama wa SSPRA wameshiriki katika maandalizi na kufanikisha uzinduzi wa kampeni hii wakishirikiana na Afsa Uhusiano wa jiji la Mwanza Bwana Joseph Mlinzi. 

Kampeni hii imezinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa jiji la Mwanza Mhandisi Erasto Ndikilo mnamo saa 4 asubuhi ambapo uzinduzi huo umebeba ujumbe mkuu wa "wazazi nipendeni" (ulinzi mtakao nipa ndio tumaini langu").Pia kampeni hii imeweza kufanikishwa na mashirika mbalimbali kama vile USAID, health Tanzania, Center for communication program, President Malaria initiative,Agakhan Health Centre,na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

Huduma ambazo zilikuwa zikitolewa ni kama vile; kupima afya bure,kupima afya ya mtoto na kupewa dawa bure, pia kupima afya ya mama mjamzito na kuwapa ushauri bure kuhusiana na "mpango binafsi wa kujifungua salama" Pia uzinduzi huu ulisindkizwa na Khalid Mohammed hali maarufu kama TID (Mnyama)kutoka jijini Dar Es salaam pamoja na kundi la uchekeshaji la Futuhi kutoka jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa Erasto Ndikilo akipewa maelekezo kuhusiana na utoaji wa huduma za afya
Wageni rasmi wakiwa meza kuu,mara baada ya ukaguzi wa mabanda ya maonyesho.

Wanachama wa SSPRA wakipanga Fliers na Brochules kwa ajili ya kuwapatia wamama wajawazito.
wanachama wa SSPRA waliofanikisha uzinduzi wa kampeni katika picha ya pamja
wanachama wa SSPRA wakipata maeezo kutoka kwa Afsa Uhusiano wa jiji la Mwanza mwenye koti la kaki

Wanachama wa SSPRA wakitoa maelezo mbalimbali katika kiwanja cha maonyesho






Mkuu wa mkoa kushto akipata maelekezo kutoka banda la Afya ya uzazi 

TID on the stage akiwaburudisha wananchi walifika katika uzinduzi huu
Kikundi cha Ngoma za asili kikimburudisha wanachi waliofia katika uzinduzi.

Kikundi cha Futuhi kikiburudisha wananchi walifika katika uzinduzi












     Afisa uhusiano wa jiji la mwanza bwana Joseph Mlinzi kushoto na Aman E. Mbwaga kulia



Saturday, November 17, 2012

TO NEW SSPRA MEMBERS OF TABORA BRANCH

Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanachama wapya wa SSPRA kutoka tawi la Tabora. Maamuzi mliyochukua ya kujiunga na SSPRA ni sahihi kabisa, Kwa moyo mkunjufu tunawakaribisha sana katika familia kubwa ya kitaaluma yenye mafanikio kila kukicha na mikakati yake ikizidi kufanikiwa kwa ujumla.

Pokeeni salamu nyingi kutoka kwa wanachama wa Mwanza, tunajipanga kuja kuwatembelea katika tawi letu  hilo jipya baada ya kuweka mambo sawa hapa chuoni SAUT-MWANZA.


Kuanzia jumatatu tarehe 19/11/2012 wale wote ambao hawajajiunga mwoneni CR wenu wa PR bwana VIRGIL MBULIGWE atakuwa na Form za kujiunga zitakazokuwa zikipatikana kwa TSH 5000 kwa ajili ya kujiunga,pia kwa wale watakao kuwa wakihitaji  Tshirt za SSPRA zitapatikana kwa Tsh. 15,000 tu.


MWENYEKITI WA SSPRA

NGONYANI CHRISTOPHER

Friday, November 9, 2012

SEMINAR SEMINAR YA INTERNET AND SURFING

WALE MEMBERS WA SSPRA NA WENGINE WENYE MAPENZI MEMA NA ASSOCIATION MNAKUMBUSHWA KWAMBA JUMAPILI SAA 6 MCHANA MPAKA SAA 10 JIONI KUTAKUAWA NA SEMINAR YA INTERNET USE AND SURFING DARASA LA M1,JITAHIDI KUJA NA LAPTOP PAMOJA NA MODEM........FIKA BILA KUKOSA, MPE TAARIFA NA MWINGINE

Thursday, November 1, 2012

MAHAFALI YA 14 CHUO CHA SAUT KUFANYIKA TAREHE 24, NOVEMBER

MAHAFALI YA KUMI NA NNE (14)
Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Mhashamu Baba Askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa anayo furaha kuwatangazia wanafunzi wote
wanaohitimu masomo chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 kwamba,
mahafali ya kumi na nne yatafanyika Jumamosi tarehe 24 Novemba 2012 katika Chuo
Kikuu cha Mtakatifu Agustino kwenye Uwanja wa Raila Odinga kuanzia saa 3.00
asubuhi.
Wahitimu wanaotarajia kushiriki mahafali hayo wanatakiwa kufanya yafuatayo:
1.Kuthibitisha ushiriki wao kwa Wakuu wa Idara kabla ya tarehe 15 Novemba
2012.
2.Wahitimu wanatakiwa kufika Chuoni tarehe 23 Novemba 2012 saa 9 mchana kwa
ajili ya taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa ajili ya
mahafali.

3.Wahitimu wote wanatakiwa kulipa shilingi 50,000 (elfu hamsini tu) kupitia
akaunti ya chuo namba 015101001461 NBC Mwanza. Shilingi 40,000 kwa ajili
ya kuazima joho na shilingi 10,000 kwa ajili ya Cheti cha Taaluma (Academic
Transcript). Wahitimu wanatakiwa kuchukua majoho tarehe 19 mpaka 22
Novemba 2013 kwenye Maktaba ya Chuo cha SAUT.

4.Majoho lazima yarudishwe ndani ya siku mbili baada ya mahafali.Vinginevyo
kutakua na faini ya shilingi 10,000 kwa kila siku itakayozidi.

5.Hosteli za chuo hazina nafasi kwa ajili ya wahitimu hivyo watatakiwa kufanya
mipango ya malazi na usafiri wenyewe.
 
WOTE MNAKARIBISHWA

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania
P .O. Box 307, Mwanza
Tel No: +25528 2552725, Fax +255 28 2550167 Email: dvcaa@yahoo.com

Friday, October 26, 2012

MEETING FOR THIRD YEAR MEMBERS OF SSPRA

TO ALL THIRD YEAR SSPRA MEMBERS, WHO MISSED THE LAST MEETING,ARE KINDLY INFORMED THAT ON TOMORROW 27/10/2012 AT M13 LECTURE HALL ,FROM 12:00PM THEY ARE SUPPOSE TO ATTEND THE MEETING. PLEASE INFORM OTHER MEMBERS ONCE YOU GET THIS INFORMATION.


HABARI NJEMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

Taasisi mpya ya binafsi inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imeanzishwa, kwa  wale ambao ndugu zao wamekosa mikopo kupitia taasisi ya serikali ya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu HESLB wanaweza kuwashauri waombe huko. taasisi hiyo inaitwa HLSSF ( Higher Learning Students Supporting Fund) 
kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii hapa http://www.hlssf.org/
  Taasisi hii inatoa huduma zingine kama ifuatavyo
  1. Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo.
  2. Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili.
  3. Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao.
  4. Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kisomi zaidi.Hii itafanikiwa kwa kuanzishwa kwa HLSSF ENTREPRENEURSHIP CLUBS kwenye vyuo mbalimbali nchini ambapo wanafunzi wanachama wa HLSSF watakutanishwa pamoja na kuweza kuandaa michanganuo bora.Hii michanganuo itatafutiwa mitaji na HLSSF ili kikundi husika cha wanafunzi waweze kuanzisha na kuendesha rasmi biashara yao.
  5. Kufanya utafiti juu ya matatizo mbalimbali yanayoikumba sekta ya elimu nchini;pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya uboreshaji wa sera husika.
  6. Kuendesha workshops,events na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwapatia elimu pana zaidi wafanyabiashara na wanafunzi juu ya maswala ya ujasiriamali, uongozi wa biashara, upatikanaji na uboreshaji wa mitaji,risk management,changamoto za soko huria n.k
  7. Kutoa ushauri kwa wanafunzi wa sekondari na vyuoni juu ya namna ya kufanya uchaguzi sahihi wa michepuo ya kusoma pamoja na kozi muafaka za kusoma kulingana na changamoto za ajira za sasa.
  8. Kutoa msaada wa kufanya maombi ya vyuo kwa njia ya mtandao(TCU ONLINE APPLICATIONS) pamoja na kufanya maombi ya mkopo wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) kwa njia ya mtandao (HESLB LOANS ONLINE APPLICATIONS).

DEBATE FORUM THIS SUNDAY

TO ALL SSPRA MEMBERS AND OTHER PUBLIC RELATIONS STUDENTS FIRST YEAR UP TO THIRD YEAR, YOU ARE KINDLY INVITED TO ATTEND A DEBATE FORUM THAT WILL BE ON SUNDAY, 28/10/2012  FROM 3:30 PM, THE TOPIC OF DISCUSSION WILL BE "PUBLIC RELATIONS IS ALL ABOUT MEDIA RELATIONS"
SO GET WELL PREPARED FOR STRONG POINTS AND LOGICAL ARGUMENTS,YOU ARE ALL WELCOME, DON'T MISS THIS CHANCE.

Friday, October 12, 2012

KIKAO KIKAO CHA SSPRA

WANACHAMA WOTE WA SSPRA MNAKUMBUSHWA KUWA TAREHE 13/10/2012 JUMAMOSI KATIKA JENGO LA MWANJONDE DARASA LA B2, KUTAKUWA NA KIKAO CHA WANACHAMA WOTE WA SSPRA KUANZIA SAA 4:00 ASUBUHI MPAKA SAA 7 MCHANA. TAFADHALI FIKA BILA KUKOSA PIA MKUMBUSHE NA MWANACHAMA MWENZIO MARA UPATAPO TAARIFA HII.