SSPRA

JOIN SSPRA TO ACQUIRE PUBLIC RELATIONS SKILLS

Monday, March 19, 2012

SSPRA WATEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI

Wanachama wa SSPRA mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Ijumaa tarehe 16/03/2012,kuanzia majira ya saa 2 asubuhi walianza safari yao ya kuelekea katika hifadhi ya taifa ya Serengeti (SENAPA) Katika kujifunza mambo mbalimbali yanayoendana na taaluma wanayosomea ya Uhusiano wa Umma na Masoko.(Public Relations and Marketing),pia katika kuendeleza sera ya utalii wa ndani ambayo imekuwa ukilegalega sana hapa nchini.

Safari hii imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwani kila kitu kilichokuwa kimepangiliwa na kamati ya Mafunzo ya nje kwa vitendo chini ya Mwenyekiti Bw.Mshana Shaabani imeweza kutekelezeka vizuri sana . Wanachama wameweza kujifunza mambo mengi sana ambayo hawakuwa wakiyafahamu kutoka kwa Afsa utalii Bw. Fred Shirima kama vile historia halisi ya Serengeti,umuhimu wa hifadhi ya Serengeti kwa Tanzania na dunia nzima,sifa za hifadhi ya Serengeti iliyonayo, vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika hifadhi hii pekee, na pia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utendaji wa kazi za uhifadhi. Pia Bw. Sadati Kimaro ambaye alikuwa ni mwongozaji wa safari (game driver) wakati wote ndani ya hifadhi alitoa maelezo mbalimbali yanayohusiana na wanyama hakuchoka kujibu maswali yote pindi alipokuwa akiulizwa na wanachama wa SSPRA.

Uongozi wa SSPRA unapenda kutoa shukrani zake za dhati kabisa kwa Uongozi wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuitikia ombi la SSPRA, Uongozi wa chuo kikuu cha Mt.Augustino kupitia idara ya uhusiano wa umma chini ya mkuu wa idara Cezalia B. Mwidima, wadhamini wa safari kampuni ya SBC Company Limited (Pepsi), Mukeshi travels, pia mlezi wa SSPRA Bw.Albert Tibaijuka.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa safari,pia Video itakuwepo baada ya kumaliza kuifanyia editing.

Maelekezo hayakukosekana

Wanachama wa SSPRA wakiwa kwenye mkutano,wakimsikiliza Afsa utalii Bw.Fred Shirima
baada ya kikao wanachama wakapata picha ya ukumbusho mahali hapa
Wadhamini wa Safari yetu pia tukawashukuru
Hao ni wanachama wa SSPRA wanaosoma mwaka wa tatu
Bwana.Fred Shirima ambaye ni Afsa Utalii akitoa maelezo juu ya serengeti

Simba akiwa amepumzika juu ya mt,hapa tulifurahi sana baada ya kumwona
Mnyama mwenye maringo kuliko wote ndani ya hifadhi
Members wakiwa hotel ya Seronera
Hotel ya Seronera mwonekano wa nje

Ilikuwa ni furaha muda wote kwa wanachama wa sspra

Mwonekano wa hoteli ya Seronera
Glory Kimaro akiwa mwenye furaha tele

bwana Aidan wa( kwanza kutoka kushoto) akiwatambia wanachama kuwa yeye ni celebrity hasipotokea kwenye picha hii basi haipendezi
Geti la kwanza la Ndabaka,hapa kabla ya kuingia ndani ya Hifadhi








kuchimba dawa pia kulihusika


Hayo sio mawe,ni viboko mahali hapa tulishangaa sana panajulikana kama hippo pool


Viongozi wakiendelea kujadiliana mambo mbalimbali wakati wa mapumziko
Hawa viboko ni wengi sana kiasi kwamba unaweza kuzani ni mawe
Hapa wanachama wa sspra wakiwa wamechoka kwa safari wakitamani kupumzika


Siku ya kwanza kabisa kufika mahali tulipolala,panaitwa Youth Hostel
Picha ya pamoja ikachukuliwa baada ya kufika Youth hostel
Tembo huyu alifanya wanachama wote wakae kimya kwani alikuwa mkubwa sana

Hapa ni kiwanja kidogo cha ndege(Air Strip) kilichopo ndani ya hifadhi
Katibu Bw.Nyanja Poti (kushoto)na Mwenyekiti Francis Moses(kulia) wa kamati ya uhusiano wa vyombo vya habari na machapisho wa SSPRA wakapata picha ya pamoja



Picha mbalimbali zilizopo katika makumbusho ya Serengeti

Game driver Sadati Kimaro na Nyanja Poti wakiwa wamepozi pia
Picha nzuri sana ya Twiga wakipishana



Mzee wa pori akiwa amepozi juu ya mti hana wasiwasi


Mwenyekiti Msaidizi wa SSPRA Bw. Medard akiwa amepiga pozi.
Bw. Frank Mashauri naye alikuwepo akiwa amepiga pozi